Yanga yapania kumaliza hasira kwa Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2020
Yanga yapania kumaliza hasira kwa Namungo Fc

Kikosi cha Yanga kesho Jumapili kitashuka kwenye uwanja wa Majaliwa Ruangwa kumenyana na Namungo Fc katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali

Namungo iliyopanda daraja msimu uliopita, msimu wake wa kwanza umekuwa mzuri kwani mafanikio iliyopata mpaka sasa hakuna aliyetarajia

Timu hiyo inayotoka jimboni kwa Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa, katika msimamo wa ligi inashika nafasi ya nne, ikiwa na alama 49

Ni alama moja tu pungufu ya Yanga inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 50

Wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Namungo wanakuwa wagumu kufungika, ni utamaduni waliojiwekea tangu walipokuwa ligi daraja la kwanza

Hata hivyo wanakutana na Yanga ambayo imetoka kujeruhiwa na KMC kwenye mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0

Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kuhakikisha wanapata ushindi ili kurejesha imani ya mashabiki kwa mabingwa hao wa kihistoria

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema pamoja na kutambua kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini hawahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’