Safari hii wataenda FIFA mapema!

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Nov 2017
Safari hii wataenda FIFA mapema!
Kwenye Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo, Msema chochote wa Simba Haji Manara amedai klabu yake ilinyimwa penalti mbili na refa Heri Sasii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC uliomalizika kwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Manara amedai refa alikwenda na matokeo yake uwanjani!

Mwanzoni mwa msimu ni huyuhuyu Manara aliyewaaminisha wanachama na mashabiki wa Simba kuwa uongozi umewasajilia timu ambayo inaweza kutangaza ubingwa hata mwishoni mwa mzunguuko wa kwanza.

Akasema kikosi cha Simba kinathamani ya zaidi ya Bil 1.3 na hivyo haoni timu ya kuwazuia kutwaa ubingwa.

Sasa baada ya kucheza michezo nane na kujikuta wameshinda minne pekee tayari wameshaanza kubadili lugha!

Alichokifanya Manara ni kujaribu kuwatia hofu waamuzi watakaochezesha michezo yao ili pengine wapindishe sheria ili mradi tu timu yao ishinde.

Kuna haja ya Bodi ya ligi kuwa makini sana na hawa watani zetu kwani wameshaona uwezekano wa kutwaa ubingwa ni mdogo sasa wanaweza kutumia mbinu zozote ili mradi kuhakikisha wanafikia lengo hilo kutuliza mzuka wa mashabiki wao.

Hakika yule aliyesema njia pekee ya wao kutwaa ubingwa ni kuliiba kombe hakukosea!

Nawaona wakianza harakati za kwenda FIFA mapemaaa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’