Tariq awapa moyo mashabiki baada ya sare

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Mar 2020
Tariq awapa moyo mashabiki baada ya sare

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc jana, mshambuliaji wa Yanga Tariq Seif amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono kwani lengo lao ni kuwapa furaha

Tariq Alifunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo kwa kuunganisha krosi iliyopigwa na Jma Abdul pamoja na kuwa alifunga bao jingine ambalo lilikataliwa na waamuzi

Mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa ameifungia Yanga mabao matatu, amesema walikosa bahati kwenye mchezo huo

"Tulitamani kuondoka na pointi zote tatu ila haikuwezekana hivyo tunashukuru tulipata hata hiyo moja kwa kuwa nayo ni sehemu ya matokeo ya mpira," alisema

"Tunawashukuru sana mashabiki wetu wote mliosafiri na sisi kutoka Dar na wale mliotoka sehemu zingine mbalimbali kuja Ruangwa kutusapoti. Tunarudi Dar kujipanga vizuri na mechi nyingine"

Baada ya mchezo huo, mechi za Yanga zimesimama kutokana na wachezaji wake saba kuitwa timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’