Kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es salaam jana usiku baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao ulipigwa juzi
Mkufunzi wa timu hiyo Luc Eymael aliwapa wachezaji mapumziko ya siku moja ambapo watarejea mazoezini hapo kesho
Afisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema Yanga itaendelea na mazoezi Jumatano kwa kuwa hawajajua mchezo wao dhidi ya Mwadui watacheza lini
"Tuna kiporo na Mwadui na hatujui tutacheza lini kwahiyo mwalimu ameona bora tuendelee na mazoezi yetu," alisema Bumbuli
ADVERTISE HERE