Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuanzia leo hakuna mtu yoyote ataruhusiwa kuhudhuria mazoezi ya klabu hiyo zaidi ya wachezaji na benchi la uundi
Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema pamoja na utaratibu huo, pia wanajadiliana na madaktari wa klabu kuandaa njia ambayo itawaweka salama wachezaji pamoja na benchi la ufundi
Licha ya Serikali kusitisha shughuli zote za michezo kwa siku 30, klabu ya Yanga inaendelea na mazoezi ambapo baada ya mapumziko ya siku moja, leo wanaendelea kujifua
Nchi karibu zote duniani zimeendelea kuchukua hatua za kiusalama kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo
ADVERTISE HERE