Yanga kujiimarisha dirisha dogo la usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2017
Yanga kujiimarisha dirisha dogo la usajili
Kwa sasa ligi kuu ya Vodacom imesimama kwa takribani wiki mbili kupisha kalenda ya mchuano ya Kimataifa ya FIFA

Habari njema ni kwamba Novemba 15 dirisha dogo la usajili kwa klabu za ligi ya Vodacom na ligi daraja la kwanza litafunguliwa na litafungwa Desenba 15.

Yanga sasa itakuwa na nafasi ya kuimarisha kikosi chake kuhakikisha inatetea ubingwa wake na kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza Februari 2018.

Katika dirisha hilo Yanga inakusudia kuimarisha kikosi chake ambapo itaanza kwa kujaza nafasi yake moja ya wachezaji wa Kimataifa.

Beki wa kati Fiston Kayembe ambaye amekuwa akifanya majaribio kwenye kikosi cha Yanga kwa miezi kadhaa anatarajiwa kulamba mkataba wa kuitumikia Yanga.

Kayembe aliichezea Yanga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC amekuwa katika kikosi cha Yanga kwa takribani miezi miwili.

Kama kila kitu kitaenda sawa Kayembe anaweza kusaini mkataba kwa wakati na kuanza kuichezea Yanga katika mchezo dhidi ya Mbeya City, Novemba 19.

Aidha kulingana na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika, alidokeza kuwa Yanga inakusudia kushusha washambuliaji wawili pamoja na winga wa kulia mwenye uwezo kama au zaidi ya Msuva.

Licha ya kukiri kuwa Pius Buswita ameanza kufanya vizuri katika nafasi hiyo, Nyika amesema Yanga inahitaji kusajili winga atakayekuwa na kasi na uwezo kama ilivyokuwa kwa Simon Msuva ili kusaidia nae pale inapobidi.

Iwapo Yanga italazimika kusajili mshambuliaji wa Kimataifa basi italazimika kuvunja mkataba wa mmoja wa wachezaji wa Kimataifa waliopo au isijaze nafasi ya beki wa kati.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
42m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’