Morrison aikana Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2020
Morrison aikana Simba

Mshambuliaji wa Yanga Benard Morrison amesema ana mkataba na mabingwa hao wa kihistoria hivyo taarifa zinazomuhusisha na Simba hazina ukweli wowote

Aidha Morrison ameeleza kushangazwa upendo mwingi anaopewa na mashabiki wa Yanga kuwa hakuwahi kuona mahali popote

"Mimi nina mkataba na klabu ya Yanga, nimekuja Tanzania kwa ajili ya Yanga hivyo hizo taarifa za mimi kwenda kujiunga na Simba hazina ukweli wowote," Morrison aliiambia Azam TV

"Mashabiki wa Yanga wananipa heshima kubwa, nimekuwa nikipokea zawadi kama fedha na hata chakula"

"Nakumbuka mchezo wangu wa kwanza Singida baada ya mchezo mashabiki walishangaza kwani walinipa fedha nyingi zinazofikia laki tano au zaidi"

"Juzi tumekwenda kucheza na Namungo, mashabiki walinipa kuku wanne.. ki ukweli upendo huu ni wa kipekee. Nimecheza Afrika Kusini, DRC lakini nakiri sikuwahi kukutana na mambo haya"

"Najihisi ni mtu mwenye deni kubwa Yanga, napaswa kufanya zaidi ili kuhakikisha naisaidia timu na kuwapa furaha mashabiki wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono wakati wote"

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’