Chirwa nae kaitwa nyumbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Mar 2020
Chirwa nae kaitwa nyumbani

Inaelezwa hesabu za Yanga ni kuongeza washambuliaji wawili matata ambao wataiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji

Mchakato wa kumrejesha Herietier Makambo anayeitumikia Horoya Ac ya Guinea tayari umeshaanza lakini pia mabingwa hao wa kihistoria wametupia jicho pale Azam Fc kwani pana mchezaji wao, Obrey Chirwa

Ndio! baada ya kuondoka Yanga, Chirwa alikwenda Misri ambako alijiunga na timu ya daraja la kwanza lakini akaikacha baada ya miezi mitatu tu

Akaomba sana afikiriwe kurudi Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu uliopita

Pamoja na uongozi wa Yanga kuridhia mshambuliaji huyo raia wa Zambia asajiliwe, akakutana na kikwazo cha kocha Mwinyi Zahera ambaye aligoma kumpa mkataba kwa kuhofia ile tabia yake ya migomo pale anapocheleweshewa haki zake

Hata usajili uliopita Chirwa alisaini mkataba mpya Azam Fc dakika za mwisho baada ya jitihada za kurejea Jangwani kukwama tena

Chirwa aliyeifungia Azam Fc mabao nane msimu huu, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu

Inaelezwa kocha Luc Eymael amevutiwa na aina yake ya uchezaji na anadhani anaweza kukinufaisha kikosi chake ambacho kitakuwa kimejaa mafundi kwelikweli

Kama mipango yote ya usajili ya Yanga itakamika, basi safu yake ya ushambuliaji itakuwa na Bernard Morrison, Ditram Nchimbi, Obrey Chirwa, Heritier Makambo na Tariq Seif

Hapa ukame wa mabao utabaki kuwa historia...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’