Pato Ngonyani, injini nyingine iliyoamshwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2017
Pato Ngonyani, injini nyingine iliyoamshwa
Wakati Yanga ikionekana kuwa kwenye kiwango bora sasa, mashabiki wengi wanawaangalia zaidi Ajib, Chirwa, Tshishimbi na hata Kamusoko kama nyota wanaoibeba Yanga.

Lakini kiraka Pato Ngonyani ni mmoja wa wachezaji walio kwenye kikosi cha Yanga ambao wamekosa bahati ya kuangaliwa kwa jicho la tatu.

Pato hufanya kazi ya ziada na kwa upande mwingine ndiyo hurahisisha kazi ya viungo washambuliaji.

Ngonyani alisajiliwa na Yanga miaka mitatu iliyopita akitokea Majimaji ya Songea. Kwenye michezo aliyocheza msimu huu amefanikiwa kuonesha kipaji alichonacho kulinganisha na umri wake.

Kwa mara ya kwanza kocha George Lwandamina alimtumia kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa saba dhidi ya Stand United na alishirikiana vyema na Tshisimbi.

Kiwango chake kwenye mchezo huo kilimshawishi kocha Lwandamina kumtumia tena katika mchezo dhidi ya Simba ingawa aliingia kuchukua nafasi ya Raphael Daudi kwenye dakika ya 60.

Ngonyani alianza kun'gara enzi za kikosi cha Hans Van Pluijm katika mashindano ya Mapinduzi miaka miwili iliyopita akicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Azam alipochezeshwa kama beki wa kati.

Pluijm pia alikuwa akimtumia kama kiungo katika mechi mbalimbali ikiwemo ya watani wa jadi, Simba.

Ngonyani anakaba kwa utulivu na akili, ni mmoja wa wachezaji walio kwenye kiwango bora ndani ya kikosi cha Yanga kwa sasa.

Bila shaka wakati huu ambao Kamusoko ni majeruhi, Lwandamina ataendelea kumuamini Ngonyani akimtumia sambamba na Kabamba Tshishimbi.

Yanga ina hazina ya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, Ngonyani ni miongoni mwa wachezaji hao.

Kama kocha Lwandamina ataendelea kumpa nafasi, Ngonyani ambaye pia anamudu vyema nafasi ya ulinzi wa kati, ni swala la muda tu atadhihirisha ubora wake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’