Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amekiri kupewa mkataba na wadhamini kampuni ya GSM lakini bado hajaurejesha
Katika mahojiano na kituo cha redio cha Wasafi, Tshishimbi amefichua kuwa mkataba wake na Yanga utamalizika mwezi wa nane
Mwaka jana Tshishimbi alisaini mkataba mpya ambao awali ilitangazwa ulikuwa wa miaka miwili
Tshishimbi amesema anawasubiri GSM kutimiza mapendekezo yake ili aweze kusaini mkataba huo na kuurejesha
Tshishimbi amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa tatu sasa
Ni mmoja ya wachezaji ambao wana mchango mkubwa na bila shaka kocha Luc Eymael ameliona hilo ndio maana akapendekeza aongezewe mkataba haraka
ADVERTISE HERE