Ni kama Yanga imedokeza jambo leo baada ya kuweka chapisho kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram linalomuelezea nahodha wake Papy Tshishimbi kama mtu wa kazi
Baada ya juzi Tshishimbi kufichua kuwa bado hajasaini mkataba wa Yanga huku akibainisha kuwa yuko tayari kujiunga na timu nyingine zaidi ya Yanga ambayo itamuhitaji na kukubaliana nayo, tetesi zimekuwa nyingi kuwa huenda akaelekea klabu ya Simba
Jana Msemaji wa Simba Haji Manara alikoleza sintofahamu hiyo kwa kumposti Tshishimbi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii huku akimwagia sifa kemkem
Katika mahojiano anayoendelea kufanya na vyombo vya habari amekuwa akitoa kauli zenye utata
Baada ya GSM kurejea Yanga, uko uwezekano wakamalizana na mwamba huyu ambaye walikuwa tayari wameanza nae mazungumzo