Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Luhago amesema uongozi wa timu hiyo utatoa taarifa rasmi kwa masuala mbalimbali yaliyojiri siku za karibuni
Dk Luhago amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani kila kitu kinakwenda sawasawa
"Kikubwa ninachoweza kusema nawaomba wana Yanga tuwe watulivu, klabu kupitia Mwenyekiti Dk Msolla tutatoa tamko rasmi, uongozi kwa pamoja tutafuatilia na taarifa rasmi kama klabu tutatoa baadaye ila wana Yanga wawe na amani kila kitu kinaenda sawa," amesema
"Yanga tuna utaratibu wetu wa kutoa taarifa na tutatolea ufafanuzi wa masuala yote ikiwemo hili la wachezaji ambao sauti zao zimevuja"
Aidha kuhusu suala la mkataba wa nahodha Papy Tshishimbi, Dk Ruhago amesema wanaendelea na mazungumzo ya kuwaongeza mikataba nyota wote ambao mikataba yao imemalizika na sio mchezaji mmoja tu
"Swala la mikataba ni binafsi hatutoweza kuweka wazi ila tuna wachezaji ambao wamemaliza mkataba na majadiliano yanaendele"
"Kumjadili mchezaji mmoja mmoja ni kama kumpa kiki, hatuwezi kujadili mchezaji mmoja mmoja tutakuja na taarifa ya wachezaji wote"
"Ni kawaida wachezaji kuibua sintofahamu kipindi cha usajili ili kuongeza thamani yao sisi hatutishwi na hilo", amesema Dk Luhago