Baada ya kufunga ndoa huko Afrika Kusini hivi karibuni, kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael amerejea kwao Ubelgiji 'kula fungate'
Mbelgiji huyo anatarajiwa kurejea kabla ya April 17 kuendelea na majukumu yake kunako mabingwa hao wa kihistoria
Baada ya kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu, mashabiki wako makini kufuatilia michakato ya usajili ya timu yao kwa ajili ya msimu ujao
Kukosa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo sio utamaduni wa Yanga kwa miaka ya hivi karibuni hivyo ni wazi msimu ujao hakuna mjadala mwingine zaidi ya kuona ubingwa unarudi Jangwani
Habari njema ni kuwa Eymael tayari alishawasilisha mapendekezo yake ya usajili kabla ya mtafaruko uliotokea baina ya Yanga na wadhamini wao GSM
Kwa ufupi, Eymael alibainisha kuwa usajili wake utaangalia zaidi mapungufu yaliyoko kwenye kikosi chake
Lakini pia alisema wachezaji wa kigeni atakaowasajili atahakikisha wanasifa na ni lazima wawe na uwezo mkubwa akimtolea mfano Bernard Morrison
Eymael amesema watapambana kuhakikisha wanashinda kombe la FA na kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao
Amesema kama watapata nafasi hiyo, watakuwa na kikosi imara ambacho kitafanya vizuri