Tulieni, Makambo mbona anakuja - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2020
Tulieni, Makambo mbona anakuja - Nugaz

Wakati mashabiki na wanachama wa Yanga wakiwa na kiu ya kuona mshambuliaji wao kipenzi, Mkongomani Heritier Makambo akirejeshwa klabuni hapo, uongozi wa klabu hiyo umesema katika usajili ujao lolote linaweza kutokea na wapo katika mchakato wa kumrejesha straika huyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema wapo katika mikakati mikubwa ya kumrejesha mshambuliaji huyo pamoja na wachezaji wengi ambao wamependekezwa na Kocha Mkuu, Mbelgiji Luc Eymael.

Alisema Kamati ya Utendaji ya Yanga na ile ya usajili kwa kupitia nguvu kubwa ya wadhamini wao, GSM na SportPesa hakuna linaloshindikana na kwamba suala la dola laki tatu kwa klabu hiyo si tatizo linapokuja suala la kumpata mchezaji anayehitajika na benchi la ufundi

"Kurejea kwa Makambo lolote linaweza kutokea kwani tayari mchakato unaendelea kwa mchezaji huyo na wengine watakuwa kuijenga Yanga na kurejea heshima yake, dola laki tatu si tatizo kwa Yanga," Nugaz amenukuliwa na Nipashe

Nugaz amesema mipango ya kamati ya Utendaji ni kufanya usajili kabambe ili msimu ujao timu iwe ya ushindani mkubwa na kuwapa raha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Mbali na Makambo, tayari uongozi wa Yanga umepanga kukaa meza mmoja na Azam FC kwa ajili ya mazungumzo kumnasa kiungo Salum Abobakar 'Sure Boy'.

Makambo aliondoka Yanga msimu uliopita baada ya kuuzwa na kusaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Horoya FC ya Guinea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’