Azam Fc yaikaribisha Yanga mezani 'kuyajenga' ya Sure Boy

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2020
Azam Fc yaikaribisha Yanga mezani 'kuyajenga' ya Sure Boy

Uongozi wa klabu ya Azam Fc umesema uko tayari kumuachia kiungo wake Abubakar Salum 'Sure Boy' kwa Yanga au timu yoyote inayomtaka kama watafikia makubaliano

Kumekuwa na taarifa Sure Boy aliyeichezea Azam Fc kwa misimu 10, ni miongoni mwa wachezaji waliopendekezwa kwenye usajili wa kocha Luc Eymael

Msemaji wa Azam Fc Zakaria Thabith 'Zaka Zakazi' amesema nyota huyo bado ana mkataba na Azam Fc lakini hilo halizuii kwao kufanya mazungumzo na timu inayotaka huduma yake

"Tunasikia kuwa kuna baadhi ya timu zinamuhitaji mchezaji wetu Salum Aboubakar, ila sisi tunachojua ni kuwa bado mchezaji huyo ana mkataba na Azam lakini hilo haliondoi uwezekano wa kumpata kwa klabu yoyote inayomuhitaji"

"Unajua kuna wakati wachezaji wanaweza kuvutiwa na mkakati fulani kutoka klabu nyingine jambo ambalo linakubalika, hivyo kama Yanga watakuja mezani tukazungumza na mchezaji mwenyewe akaridhia basi sisi hatuna kipingamizi tutaruhusu aende," alisema

Baada ya sakata la Gadiel Michael, Azam Fc na Yanga kwa sasa zimerejesha mahusiano mema ya kibiashara katika masuala ya usajili

Mwezi Januari Yanga ilimsajili Ditram Nchimbi kutoka Azam Fc ingawa alikuwa akiitumikia kwa mkopo Polisi Tanzania

Miaka ya nyuma Azam Fc iliwahi kuwasajili 'kibabe' nyota wa Yanga Frank Domayo na Didier Kavumbagu usajili ambao uliwakera mabosi wa Yanga ambao walikuja kumsajili kibabe Gadiel Michael usajili ambao ulisababisha mvutano baina ya timu hizo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’