Kiiza aikumbuka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2020
Kiiza aikumbuka Yanga

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Hamis Kiiza ambaye aliwahi kutamba kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kati ya mwaka 2010 na 2014, amesema anatamani kurejea Tanzania kuitumikia tena Yanga

Kiiza aliyeichezea Yanga kwa misimu mitatu alifanikiwa kufunga mabao 56, kwa sasa anaitumikia klabu ya Proline Fc ya huko Uganda

Msimu wa 2016/17, Kiiza aliitumikia Simba kwa msimu mmoja lakini amesema katika timu tisa ambazo amezitumikia, anaikumbuka zaidi klabu ya Yanga

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, amesema bado yuko fiti na anatamani siku moja arejee Tanzania aitumikie tena Yanga

"Nimecheza katika timu tisa tangu nianze soka la ushindani, lakini kote huko siwezi kuisahau Yanga ambayo ndio iliyonifanya nitambulike sehemu kubwa duniani," amesema Kiiza

"Bado nacheza mpira, sina mpango wa kustaafu hivi karibuni  mipango yangu siku moja nirudi Tanzania kucheza timu ya Yanga kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ni jinsi wanavyothamini wachezaji wao katika hali zote"

Kiiza ni mmoja wa washambuliaji wa kigeni ambao walikubalika sana na mashabiki wakati wakiitumikia Yanga

Hata hivyo kwa sasa haonekani kuwa na nafasi ya kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria ambao wako kwenye mchakato wa kuiimarisha timu yao kwa ajili ya msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’