Viingilio mchezo wa Singida United vs Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2017
Viingilio mchezo wa Singida United vs Yanga
Kesho Jumamosi, Novemba 04 nyasi za uwanja wa Namfua mkoani Singida zitawaka moto pale kikosi cha Singida United kitakapowakaribisha mabingwa wa VPL kwa misimu mitatu mfululizo Yanga.

Licha ya kuwa imepanda daraja msimu uliopita, Singida United imejipambanua kuwa ina malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Hans van Pluijm kocha wa zamani wa Yanga ndiye mkufunzi wa timu hiyo kwa sasa.

Sasa kuushuhudia mchezo huo wa kipekee, kwa wale wa jukwaa kuu tiketi zinapatikana kwa Tsh 10,000/- huku wale wa mzunguuko wakizipata tiketi zao kwa Tsh 7,000/-

Mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni na utaonyeshwa LIVE na Azam TV. Kwa wale wa mikoani watakuwa na fursa ya kuushuhudia mubashara kupitia runinga zao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’