Eymael ameniongezea kujiamini - Makapu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2020
Eymael ameniongezea kujiamini - Makapu

Mlinzi wa kati wa Yanga, Said Juma Makapu amesema mkufunzi wa timu hiyo Luc Eymael amekuwa akimpatia mbinu zinazomfanya kucheza michezo mingi ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila presha ikiwa ni tofauti na makocha waliopita huko nyuma.

Tangu kocha Eymael amejiunga na mabingwa hao wa kihistoria katikati ya msimu huu, amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza na kutengeneza muunganiko mzuri sehemu ya ulinzi pamoja na Lamine Moro, huku akimuweka benchi beki mkongwe Kelvin Yondani.

Akizungumza Dar es Salaam jana Makapu alisema amefundishwa na makocha wengi ndani ya kikosi hicho tangu alipojiunga akitokea Shangani FC ya Zanzibar lakini Eymael ndiye mwalimu anayempatia uhuru wa kucheza na kujiamini kabisa.

Makapu amemsifia Yondani kuwa ni beki bora na amekuwa akijifunza mbinu tofauti namna ya kukabiliana na washambuliaji wakali na kwamba kitendo cha kukaa kwake benchi sio kwamba kiwango chake kimeshuka.

"Pamoja na kupewa nafasi ya kuanza bado Yondani ana kiwango kikubwa kuliko mimi kutokana na uzoefu wake wa kucheza michezo tofauti ikiwemo kushiriki michuano ya kimataifa Afrika," alisema Makapu

Makapu alisema wakati anajiunga na kikosi hicho alianza kufundishwa na kocha Marcio Maximo na baadaye makocha kama Hans Van der Pluijm, George Lwandamina na Mwinyi Zahera lakini wote hao walikuwa wanamuweka zaidi benchi.

Ndani ya kikosi cha Yanga Makapu ni miongoni mwa wachezaji watatu waandamizi pamoja na Yondani na Juma Abdul baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu kuwashinda nyota wengine waliopo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’