Siku za karibuni aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amekuwa akitoa maoni tofauti kuhusu michakato ya usajili inayofanywa na mabingwa hao wa kihistoria
Alianza kwa kudai kuwa mshambuliaji David Molinga amepata timu DR Congo hivyo hawezi kuendelea kuichezea Yanga
Wiki iliyopita baada ya kuibuliwa taarifa kuwa mabingwa hao wa kihistoria wako kwenye mchakato wa kumrudisha mshambuliaji Herietier Makambo, Zahera aliibuka na kudai mshambuliaji huyo hawezi kurudi Tanzania kuichezea Yanga
Aidha Mcongomani huyo alisema kuwa Yanga haina ubavu wa kumlipa mshahara anaopata Horoya lakini pia haina fedha za kuvunja mkataba wake wa miaka miwili
Hata hivyo pengine asichofahamu Zahera ni kuwa kwa sasa mambo yamebadilika Yanga baada ya GSM kuchukua jukumu la kuisimamia timu
Tangu GSM wachukue jukumu hilo mwezi Januari, hakuna tena malalamiko ya mishahara huku wakifanya usajili ulioifufua Yanga aliyokuwa ameizika yeye
GSM ndio wanaosimamia mchakato wa kumsajili Makambo na wenyewe wamesema kama dau lake ni chini ya dola laki tano (Bilioni moja) basi watamsajil
Zahera asitoe kauli za kuikatisha tamaa Yanga, yeye alipewa nafasi ya kufanya kila kitu lakini alishindwa
Kwa sasa Zahera wakati wake umepita, ni vyema akatulia awaache wenzie nao wafanye kazi