Wananchi wameaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona ambao umeendelea kusababisha hofu kwa maisha ya watu kote duniani
Jana Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza uwepo wa wagonjwa wengine wapya wanne wa maambukizi ya virusi vya coronahapa nchini
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mapema jana, kati ya wagonjwa hao wanne, wawili wanatoka Tanzania Bara na wawili wanatoka Zanzibar
βWizara ya Afya imethibitisha kuwepo kwa kesi mpya nne za maambukizi ya virusi vya corona (COVI-19) zilizopatikana Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar na kufanya kuwepo kwa jumla ya kesi 24 zilizoripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huu nchini,βΒ ilisema sehemu ya taarifa hiyo
Serikali imetoa msisitizo kwa Wananchi kusikiliza maelezo ya wataalamu wa Afya kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19 hususan kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka
Aidha, Wananchi wamesisitiziwa kuzingatia maelezo mengine yanayohusu kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kukaa umbali usiopungua mita moja kati ya mtu na mtu
Β