Kampuni ya GSM imesema kuwa itahakikisha mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uwendeshaji wa klabu ya Yanga unakamilika mwezi ujao kama ulivyopangwa
Akizungumza na wanahabari mapema leo katika Mkutano ambao waliufanya pamoja na Yanga, Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wanaunga mkono jitihada za 'transformation' zinazofanywa na uongozi wa Yanga
"Tunafahamu mwezi ujao uongozi wa Yanga umetangaza kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji. Tunashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha mchakato huo unakamilika"
"Kwani tunaamini klabu ya Yanga itafungua ukurasa mpya. Huo utakuwa mwanzo wa mafanikio makubwa kwa klabu yetu, sisi tutakuwa mfano kwa wengine," amesema
Wadau mbalimbali wa klabu ya Yanga wanaipiga 'chapuo' GSM ijitose kuwa wawekezaji rasmi wa klabu hiyo baada ya mabadiliko kufanyika
Zipo dalili njema zinazoashiria GSM huenda wakawa miongoni mwa makampuni yatakayojitokeza kuwekeza Yanga