GSM kutumia Mamilioni usajili wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2020
GSM kutumia Mamilioni usajili wa Yanga

Imezoeleka kwa vilabu vya hapa nchini, havisajili wachezaji wenye mikataba, mara nyingi husubiri mikataba ifike mwisho kisha kusajili wachezaji walio huru

Hata hivyo Yanga kupitia wadhamini/wahisani wao GSM, usajili wa kuelekea msimu ujao watafanya mambo tofauti

Imeelezwa GSM walimpa mkufunzi wa Yanga Luc Eymael uhuru wa kupendekeza wachezaji anaotaka wasajiliwe bila ya kujali kama mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu au la

Mabilionea hao wamejipanga kutumia 'fedhwa' kufanya usajili wa maana na pengine kwa mara ya kwanza kwenye usajili ujao wa Yanga inaweza kushuhudiwa mchezaji akanunuliwa hata kwa Tsh Milioni 500 au zaidi ili mradi tu awe na sifa na pia awe amehitajika na kocha

Na ndio maana pamoja na kufahamu mshambuliaji Heritier Makambo kuwa na mkataba Horoya AC, klabu ya Yanga imeanza mazungumzo na klabu hiyo ili kuipa sahihi ya nyota huyo aliyejitengenezea jina licha ya kuitumikia Yanga kwa msimu mmoja tu

Jana Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisema kampuni hiyo itashirikiana na uongozi wa Yanga kufanya usajili kabambe ambao wana uhakika utawapa ubingwa msimu ujao

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’