Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Tanzania imeanza kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ya ndani kuanzia maambukizi yaliyopatika tarehe 08/04/2020.
Amesema kuwa tahadhari kubwa inahitajika katika kuhakikisha kuzuia kuendelea kwa maambukizi ya kijamii itasababisha kuongezekana kwa kasi ya maambukizi katika jamii.
Ameyazungumza hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini katika kujadiliana namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi ya Corona nchini.
Ameongeza kuwa Serikali itatangaza hivi karibuni wananchi kuchukua tahadhari kwani tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaweza kusambaa na kuambukizwa kwa njia ya hewa hivyo maelekezo ya kutumia barakoa yatatolewa ili kuondokana na maambukizi.
"Tafiti zimeonesha kuna uwezekano wa Virusi vya Corona vinaweza kuenezwa kwa njia ya hewa hivyo tutaleta muongozo wa kuanza kutumia Barakoa (Mask) kwa jamii ili kuzuia maambukizi kuenena kwa njia ya hewa' alisema
Aidha amewataka viongozi wa dini kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwalinda watoto kutowaruhusu Watoto kuzurula na kuhangaika ovyo mitaani ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
"Imani ya watanzania wengi kufikiri kuwa hatuwezi kupata maambukizi ni suala sahihi tunaweza kupata maambukizi kama watu wengine wanavyopata"