GSM wanavyoifanya Yanga kuwa ya kisasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2020
GSM wanavyoifanya Yanga kuwa ya kisasa

Jana Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM Mhandisi Hersi Said alibainisha kuwa juu ya mkataba wa kutengeneza na kusambaza jezi za klabu ya Yanga, wamesaini mkataba mwingine na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kutengeneza bidhaa nyingine za klabu hiyo

Mkataba huo wa mwaka mmoja, utawawezesha kutumia nembo ya Yanga kutengeneza bidhaa nyingine kwa niaba ya mabingwa hao wa kihistoria

Bidhaa hizo ni pamoja na skafu, bangili, fulana za kike na za kiume kuanzia za vijana wadogo hadi watu wazima, viatu, vikombe na vitu vingine mbalimbali

Hersi alisema kuwa Yanga itanufaika kwa kujiongezea mapato kutokana na mradi huo

Hii ni habari njema kwa Yanga ambayo kwa muda mrefu imekuwa na ndoto ya kuzalisha bidhaa hizo kwa ajili ya mashabiki wake

Huu ndio mwanzo wa Yanga ya kisasa, kwani wakati mchakato wa mabadiliko ukiendelea, haya yanayofanyika yanaashiria neema huko mbeleni

Klabu zote kubwa duniani zina utaratibu huu, ni muhimu kunufaika na wingi wa mashabiki ambao timu inakuwa nao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’