Utaratibu wa kuweka kambi nje ya nchi unarudi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2020
Utaratibu wa kuweka kambi nje ya nchi unarudi

Wadhamini wa klabu ya Yanga kampuni ya GSM wamepanga kuipeleka timu hiyo nje ya nchi kuweka kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao, imefahamika

Hata hivyo uamuzi huo utategemea na mwenendo wa mapambano ya ugonjwa ya corona ambao umesitisha shughuli zote za michezo duniani

Mmoja wa viongozi waandamizi wa Yanga amefichua kuwa GSM wamejipanga kufanya mambo makubwa kuelekea msimu ujao ikiwa ni pamoja na kurejesha utaratibu wa kuweka kambi nje ya nchi

"Maandalizi ya mwaka huu yatakuwa bab'kubwa, wadhamini wetu wameahidi kuipeleka timu nchi yoyote ambayo benchi la ufundi litapendekeza. Kama hii shida ya corona itakuwa imemalizika, basi mwaka huu timu itaenda kuweka kambi nje ya nchi," kilifichua chanzo

Tangu alipojiuzulu aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji, mabingwa hao wa kihistoria walishindwa kuendeleza utaratibu wa kuweka kambi nje ya nchi kutokana na uhaba wa fedha

Kwa misimu mitatu iliyopita, Yanga imekuwa ikiweka kambi mkoani Morogoro

Enzi za Manji Yanga iliwahi kuweka kambi nchi za Ubelgiji na Uturuki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’