Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael kwa mara nyingine amelazimika kufuta safari yake ya kurejea nchini kutokana na janga la corona
Eymael ambaye alirejea kwao huo Ubelgiji kufunga ndoa, ilikuwa aondoke nchini humo leo na pengine angewasili Tanzania keshokutwa Jumatano
Hata hivyo baada ya Serikali ya Tanzania kufuta safari zote za ndege kutoka nje ya nchi, Eymael atalazimika kusubiri mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa
"Sasa uwanja wa ndege wa kimataifa nchini Tanzania umefungwa. Tunapaswa kuahirisha kurudi tena Tanzania, Ndugu kaa nyumbani, kaa salama na familia yako na kwa wachezaji wangu, wasisahau kufanya mazoezi yao binafsi," amesema Eymael
ADVERTISE HERE