Mmoja wa wadhamini wa klabu ya Yanga kampuni ya GSM ambayo imejitosha kusimamia mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo, wametangaza kuwa wako mbioni kusaini mkataba wa ushirikiano na Ligi Kuu ya Hispania maarufu La Liga
Lakini kubwa zaidi Yanga pia itasaini mkataba na moja ya klabu kongwe inayoshiriki La Liga ambayo ni miongoni mwa vilabu vinavyowania nafasi nne za juu katika ligi hiyo
Kulingana na Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, Mkataba huo utaiwezesha Yanga na klabu hiyo (haijatajwa) kuweza kushirikiana idara zote za uendeshaji, program za mazoezi, vyumba vya kubadilishia nguo, aina ya vifaa vitakavyotumika mazoezini, ufundishaji na pia kitengo cha scouting ya wachezaji
Hersi amesema anaamini kusainiwa kwa mikataba hiyo kutainufaisha Yanga na anaamini itakuwa klabu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kutumia utaratibu huo
Aidha Hersi amesema mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na mabadiliko ya kikosi cha timu ambapo amefichua kuwa msimu ujao Yanga itakuwa na kikosi bora
"Msimu ujao tumejipanga kuwa na timu ya ushindani, dirisha litakapofunguliwa mchezaji yeyote ambaye Mwalimu atamuhitaji tutamsajili bila kujali daraja lake," Hersi aliiambia eFM