Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael yuko makini kufuatilia program za mazoezi alizowaachia nyota wake wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na janga la corona
Mbelgiji huyo ameshindwa kurejea nchini kutokana na changamoto ya usafiri, anawafuatilia wachezaji mmoja mmoja kupitia mtandao wa WhatsApp
Inaelezwa wakati mwingine huwaagiza nyota wake kurekodi na kumtumia vipindi vya vya mazoezi wanayofanya
Eymael aliyetua Yanga mwezi Januari 2020 kutoka klabu ya Black Leopards ya ligi kuu ya Afrika Kusini, hataki nyota wake wawe wameshuka viwango pale ligi itakaporejea
Makocha wengi wa timu za ligi kuu wana wasiwasi ligi itakaporejea wachezaji hawatakuwa na hali nzuri ya kimchezo
Hivi karibuni kocha wa Ndanda Fc Abdul Mingange aliiomba TFF kuvipa vilabu angalau wiki mbili za kujiandaa pale ligi itakaporejea
Eymael anapiga hesabu zaidi ya michuano ya kombe la FA ambapo mpango uliopo ni kuhakikisha Yanga inatwaa taji hilo ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao