Kiungo Mkenya atamani kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2020
Kiungo Mkenya atamani kutua Yanga

Huo upepo wa GSM unavuma kila pembe ukanda huu wa Afrika Mashariki hali inayowafanya wachezaji kutamani kujumuishwa kwenye 'project' ya kuijenga Yanga inayofanywa na matajiri hao walioapa kutengeneza kikosi cha maangamizi

Kiungo mshambuliaji wa Kariobang Sharks, Sven Yidah imeeleza kutamani kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria

Yidar ni miongoni mwa wachezaji ambao tetesi ziliwahusisha kujiunga na Yanga mapema tu lakini kocha Luc Eymael akakanusha kumfuatilia nyota huyo

Kiungo huyo ameeleza kuvutiwa na ligi ya Tanzania hasa Yanga ambayo ameifahamu kupitia historia yake na mechi mbili alizocheza nayo kwenye michuano ya Sportpesa na kilele cha wiki ya Mwananchi kabla ya msimu huu kuanza

"Ligi ya Tanzania ina msisimko kuliko huku Kenya. Naifahamu Yanga ni klabu yenye historia kubwa, nimecheza nao mara mbili. Kama wakinitaka na tukafikia makubaliano niko tayari kujiunga nao. Pale Yanga nitafutahi kucheza na yule nahodha wao (Tshishimbi) na Fei Toto," alisema

Hata hivyo kocha Eymael ameeleza kutomfahamu kiungo huyo huku akibainisha sio miongoni mwa wachezaji aliopendekeza wasajiliwe na timu yake

"Huyo mchezaji simfahamu, labda nipate nafasi ya kumfuatilia lakini siwezi kupendekeza mchezaji nisiyemfahamu," amesema

"Kabla sijaondoka Tanzania, nilipendekeza orodha ya majina tofauti, mchezaji mmoja au wawili kutoka Rwanda, mmoja kutoka Ubelgiji na mwingine kutoka Burundi. Pia mchezaji mmoja au wawili kutoka Misri na mmoja kutoka Ghana"

Inaelezwa Yanga iko karibu kumsaini kiungo kutoka klabu ya Rayon Sport ya nchini Rwanda, Ally Niyonzima

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’