GSM yafafanua mgawo wa Mil 200 za bonasi ushindi dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2020
GSM yafafanua mgawo wa Mil 200 za bonasi ushindi dhidi ya Simba

March 08 2020 ilikuwa siku muhimu kwa wachezaji na mashabiki wa Yanga baada ya timu hiyo kuwalaza na viatu watani zao Simba kwa ushindi wa bao 1-0, bao lililowekwa kambani na Bernard Morrison

Ushindi huo ulimaliza ufalme wa miaka minne wa klabu ya Simba kwenye mechi za 'derby'. Lakini pia ulikuja na neema kwa wachezaji baada ya moja ya wadhamini, kampuni ya GSM kutoa bonas ya kitita cha Tsh Milioni 200

Hata hivyo mgawo wa fedha hizo nusura ulete mtafaruko kufuatia baadhi ya wachezaji kulalamika kuwa walitengwa

Mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Mhandisi Hersi Saidi ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu uliotumika kuzigawa fedha hizo

Hersi amesema wamekuwa wakitumia utaratibu huo tangu walipoanza kutoa bonasi kwa kila ushindi mwezi Novemba 2019

Bosi huyo wa GSM amesema utaratibu uliotumika kugawa bonasi ulihusu wachezaji waliohusika moja kwa moja katika mchezo

Kwa maana, wachezaji 18 waliokuwa kwenye kikosi siku ya mchezo, na wachezaji wengine nane ambao walikuwa sehemu ya timu iliyoingia kambini

"Tulikubaliana kuwa timu itakayoshinda ndio itapata winning bonasi na hilo sio tu katika pambano lile dhidi ya Simba, ila utaratibu huo tuliuanza tangu Novemba mwaka jana na Yanga ikishinda inapata winning bonasi," alisema

"Wachezaji waliokuwa kambini kujiandaa na pambano dhidi ya Simba walikuwa 26, na wale waliokuwa kambini ndio waliotakiwa kupata bonasi hiyo, ambapo 14 waliocheza katika mchezo ule bila kujali alicheza muda gani, kila mmoja alipewa Sh milioni 10 na jumla ilikuwa milioni 140"

"Milioni 60 ziliobaki ziligawiwa kwa wachezaji wanne waliokuwa benchi na sita waliokaa jukwaani, pamoja na benchi la ufundi lenye makocha tisa ukimuondoa Kocha Mkuu, Luc Eymael, ambaye yeye katika milioni 60, alipewa milioni 10"

"Wachezaji hao waliokaa benchi na wale wa jukwaani, kila mmoja alipewa Sh milioni 2.5 wakati benchi la ufundi, kila mmoja alipewa Sh milioni 3.5 pamoja na kocha msaidizi, Charles Mkwasa, ambao walikamilisha kiasi cha Sh milioni 50.

"Kwa wachezaji ambao hawakuwepo kabisa hata katika kambi, wenyewe hawakupata chochote," alifafanua

Hersi aliongeza kuwa utaratibu huo ndio walikubaliana kati ya GSM, kocha, nahodha na wachezaji jinsi ya kugawana bonasi zote pale Yanga itakaposhinda mchezo wowote ule

Na kuwa hata mechi za nyuma mchezaji ambaye hatakuwa kambini kwa ajili ya mchezo unaokuja na timu ikishinda, hatapata kitu hiyo ni sehemu ya makubaliano.

Hivi karibuni sauti za mshambuliaji David Molinga na kiungo Abdulaziz Makame zilivuja kwenye mitandao ya kijamii wakilalamika kutopata mgawo

Nyota hao hawakuwa sehemu ya timu iliyoingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’