Eymael ataja sababu ya kusajili kiungo mkabaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2020
Eymael ataja sababu ya kusajili kiungo mkabaji

Pamoja na nahodha Papy Tshishimbi kufanya vyema eneo la kiungo mkabaji, kocha Luc Eymael ametaja sababu ya kusajili kiungo mkabaji mwingine

Inaelezwa Yanga iko karibu kumsajili kiungo wa Rayon Sport Ally Niyonzima huku mabingwa hao wa kihistoria wakihusishwa na nyota wa Mtibwa Sugar Abdulkarim Humud

Eymael amesema anahitaji kiungo ambaye anamudu vyema nafasi hiyo kwani waliopo wana changamoto ya kusahau majukumu yao ambayo ni kuilinda safu ya ulinzi

"Msingi wa timu siku zote unaanzia chini, nikimaanisha namba sita ambaye kama yeye akishindwa kutimiza majukumu yake vizuri, basi lazima makosa yatakuwa mengi golini kwetu"

"Kama umekuwa ukifuatilia mechi ambazo tumekuwa tukipoteza makosa mengi yamekuwa yakifanywa na viungo wakabaji namba sita wamekuwa hawatimizi vema majukumu yao ya uwanjani"

"Hivyo, basi nimepanga kusajili kiungo mkabaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi hiyo ya kiungo ambaye hatakuwa akihama katika eneo lake la katikati," Eymael amenukuliwa na gazeti la Championi

Eymael amefichua mpango wake wa usajili ambapo Mbelgiji huyo amepanga kusajili wachezaji 10 wapya, wanne wakiwa wa kigeni

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’