Yondani atamalizia maisha yake ya soka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2020
Yondani atamalizia maisha yake ya soka Yanga

Mkataba wa nahodha wa zamani wa Yanga, mkongwe Kelvin Yondani unamalizika mwishoni mwa msimu hata hivyo mwamba huyo wa ziwa huenda akaongezwa mwaka mmoja

Kwa sasa kwenye kikosi cha Yanga, Yondani ndiye mchezaji aliyedumu kwa muda mrefu zaidi (miaka nane)

Kutokana na umri wake kuendelea kumtupa mkono, hana muda mrefu sana wa kuendelea kusakata kabumbu

Inaelezwa kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael alipendekeza asakwe mbadala wake, hata hivyo mabosi wa Yanga wameweka msimamo wakitaka kumuona Yondani akistaafu kwa heshima Yanga

Pamoja na kuwa mmoja wa mabeki bora kuwahi kutokea nchini Tanzania, Yondani alikubali kucheza Yanga hata katika zile nyakati ngumu ambazo wachezaji wazuri walikuwa wakikimbilia timu nyingine

Baada ya Nadir Haroub kustaafu kwa heshima Yanga, Yondani atapewa nafasi hiyo pale atakapoamua kustaafu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’