Makocha wa makipa wakasome - Ndayiragije

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2020
Makocha wa makipa wakasome - Ndayiragije

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars ‘, Ettiene Ndayiragije, amewataka makocha wa makipa wasome ili kujua misingi bora ya kuwatengeneza makipa bora wanaohitajika kulingana na soka la kisasa na kuacha kutumia uzoefu kufundisha.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ndayiragije alisema makocha wengi wa makipa waliopo hawaendi darasani kuongeza elimu, bali wamekuwa wakifundisha kwa uzoefu kwa sababu walipitia kazi hiyo wakati kuna mambo mengi muhimu wanakosa kulingana na soka la kisasa.

“Kuna changamoto kwa makocha wetu wa makipa waliopo, kuna vitu wanakosa vya kufundisha makipa ili kuwa washindani, kwani wengi waliopo wanatumia uzoefu, wanahitaji kwenda kozi kujifunza baadhi ya mambo muhimu kwa makipa na kuwatengeneza kuwa bora,” alisema.

Hata hivyo, Ndayiragije alisema hapati ugumu wa kuchagua makipa wa kutumikia timu ya taifa kwa sababu wenye uwezo na ushindani ni wachache na mbaya zaidi wapo wanaovuma msimu mmoja baadaye wanapotea.

Alisema kuna vitu vingi makipa wanapaswa kujifunza hasa mbinu za kuboresha kazi zao kutoka kwa makocha wao kabla ya kuitwa kwenye timu ya taifa ili kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Aidha, alisema makipa waliopo wanakosa ushindani ndio maana alipomrejesha Juma Kaseja ilisaidia wengine kuanza kujituma na kurudi katika kiwango bora chenye ushindani.

Alisema makipa wengi kwa sasa wamebadilika na kucheza soka la kisasa na wengine wakionesha umakini mkubwa katika kuhimiza wachezaji wao kulinda maeneo yao.

Ndayiragije alisema kuna changamoto ya kupata makipa wanaohitajika hasa kwa kuzingatia vigezo kama urefu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’