Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetoa taarifa kuwa sampuli zilizopimwa katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kati ya tarehe 18 hadi 20 April, 2020 zimethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya 84 wenye maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini.
Kati yao, wagonjwa 16 waliotolewa Taarifa na Waziri wa Afya wa Zanzibar leo tarehe 20 April 2020
Kwa upande wa Tanzania Bara idadi ya wagonjwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni kama ifuatavyo; Dar es salaam (33), Arusha(4), Mbeya(3), Kilimanjaro (3), Pwani(3), Tanga(3), Manyara (2), Tabora(1), Dodoma (3), Ruvuma (2), Morogoro(2), Lindi(1), Mara(1), Mwanza (3), Mtwara(1), Kagera(1) na Rukwa (2)

ADVERTISE HERE