Sare zatawala ligi kuu ya Vodacom

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2017
Sare zatawala ligi kuu ya Vodacom
Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2017-18 imeanza kwa ushindani wa hali ya juu kila timu ikionekana kujipanga.

Idadi kubwa ya michezo imemalizika kwa sare huku vipigo vikubwa pekee vikiwa mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting (7-0) na ule wa Stand United dhidi ya Yanga (0-4).

Azam FC iko kileleni wakati huu kabla ya michezo mingine ya kukamilisha mzunguuko wa tisa.

Imejikusanyia alama 19 kati ya alama 27 na hivyo kupoteza alama nane kutoka michezo tisa mpaka sasa.

Hata kama Simba itapata ushindi dhidi ya Mbeya City haitabadili takwimu hizo kwani itafikisha alama 19 pia.

Msimu huu umekumbwa na 'ukata' wa ushindi pengine hii ni dalili njema kuonyesha soka la Tanzania katika ngazi ya vilabu sasa limeanza kuimarika.

Kwa miaka mingi vilabu vya Simba na Yanga vimetawala soka la Tanzania lakini kwa hali ilivyo msimu huu yanaweza kutokea maajabu.

Simba iliyojinasibu kutumia pesa nyingi kwenye usajili kuliko timu yoyote inayoshiriki VPL, imejikuta ikiwa katika wakati mgumu kupata matokeo kama ilivyo kwa timu nyingine.

Dalili zinaonyesha msimu huu bingwa huenda akajikusanyia alama chache zaidi huku swala la mabao linaweza tena kuamua hatma ya ubingwa.

Mpaka sasa timu zimekuwa zikipokezana usukani wa ligi kwa tofauti ya mabao hivyo timu itakayofunga mabao mengi huenda ikanufaika mwishoni mwa msimu.

Ni vyema wakati huu Yanga ikatumia vyema dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Novemba 15 kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Ni muhimu kwa benchi la ufundi kuboresha zaidi kasi ya upachikaji mabao kwani huenda bingwa akaamuliwa kwa tofauti ya mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Ni muhimu pia kwa Yanga kuhakikisha inashinda michezo yake yote ya nyumbani ili kujikusanyia alama nyingi iwezekanavyo.

Msimu huu michezo ya mikoani itakuwa migumu zaidi hasa kwenye mzunguuko wa pili wakati mvua zitakapokuwa zimepamba moto.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’