Vicenti Bossue 'Kaka jambazi' ni beki ambaye nadhani mashabiki wengi wa Yanga bado hawajamsahau kutokana na umahiri wake
Bossue raia wa Togo alisajiliwa na Hans van Pluijm mwaka 2015 wakati huo akiwa kocha wa Yanga
Mashabiki walichelewa sana kumuelewa mwamba huyu kutoka Togo lakini pale walipomuelewa, walitamani kumuona dimbani kila mabingwa hao wa kihisoria walipocheza
Ni beki mtaratibu ambaye hana papara, urefu na umbo lake ilikuwa silaha muhimu katika kudhibiti washambuliaji watata
Bossue alipendelea zaidi kuvaa jezi namba tisa, pengine ni kutokana na umbo lake, ni rahisi sana kudhani ni mshambuliaji

Nahodha Msaidi wa Yanga Juma Abdul amesema kama atapewa nafasi ya kupendekeza mchezaji mmoja arudishwe, basi atamchagua beki huyo ambaye wakati huo alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Togo
"Mchezaji ambaye natamani kumuona tena kwenye kikosi cha Yanga ni Vicent Bossue. Jamaa alikuwa anajua sana..," alisema
Hata hivyo Abdul amesema wachezaji waliopo Yanga sasa sio wabaya, wanachohitaji ni kukaa pamoja kwa muda ili waweze kutengeneza kikosi imara zaidi
"Ukiangalia kwa sasa tunavyocheza ni tofauti na tulivyoanza. Kama isingekuwa corona nadhani tungekuwa bora sana wakati huu kwani timu ilikuwa ikiimarika siku hadi siku"