Mlinzi wa Polisi Tanzania Rajab Zahir amesema mshambuliaji wa Yanga Tariq Seif Kiakala ni mmoja wa washambuliaji bora ligi kuu ya Vodacom, ni mchezaji anayehitaji umakini mkubwa kuweza kukabiliana nae
Zahir ambaye amewahi kuitumikia Yanga, amewataja Tariq na Meddie Kagere kuwa ndio washambuliaji anaowahofia zaidi
"Tariq ni mchezaji anayehitaji maarifa zaidi kumkaba kwani ni mshambuliaji mjanja mjanja," Zahir alinukuliwa na Mwanaspoti
"Muda wote huwa hatulii sehemu moja ndani ya uwanja na anahitaji umakini ili kuhakikisha hapati nafasi ya kufunga"
"Angalia mabao anayofunga, unaona kabisa mabeki walimsahau na ndio mchezo wake hivyo unahitaji sana kuwa makini kumkaba mara nyingi unajikuta unapata lawama kwani ukizubaa tu kakufunga. Ni mshambuliaji mjanja mjanja, ana mambo mengi zaidi ya kufunga," alisema
Tariq alitua Yanga usajili wa dirisha dogo akitokea nchini Misri alikokuwa anacheza soka la kulipwa
Kabla ya kutimkia Misri, Tariq amewahi kuzitumikia Stand United na Biashara United