Beki chipukizi wa Yanga SC, Abdallah Hajji 'Ninja' ni miongoni mwa wachezaji 30 walioitwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Zanzibar, maarufu Zanzibar Heroes kwa ajili ya michuano ya CECAFA Challenge mwezi ujao.
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza kurudi kwa Kombe la Challenge na Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman 'Morocco', ametangaza kikosi cha awali, akichukua nyota kadhaa wanaocheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa CECAFA, mashindano hayo yatafanyika kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya.
Wachezaji hao watafanya mazoezi ya pamoja na baadae kuchujwa ili kupata kikosi cha mwisho kitakachokwenda kujaribu kutwaa ubingwa wa pili kwa Zanzibar katika historia ya mashindano hayo.
Wachezaji wengine wa Yanga walioitwa katika kikosi hicho ni Haji Mwinyi na Matheo Antony

ADVERTISE HERE