Wachezaji wa Yanga Feisal Salum, Adeyum Saleh na Abdulaziz Makame 'Bui' wako visiwani Zanzibar wakiendelea na mazoezi binafsi wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na janga la corona
Nyota hao wameeleza kujifua angalau mara mbili kwa siku ili kuhakikisha wanakuwa sawa pale ligi itakaporejea
Ligi imesimama kwa takribani siku 40 sasa baada ya Serikali kusitisha shughuli zote za michezo nchini kutokana na ugonjwa huo
Shirikisho la soka nchini (TFF) limesema kuwa linasubiri mwongozo wa Serikali kabla ya kuweka hadharani mustakabali wa ligi
ADVERTISE HERE