Balama apewa 'mchongo' aweze kutimkia Ulaya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2020
Balama apewa 'mchongo' aweze kutimkia Ulaya

Kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama ametakiwa kuongeza juhudi ili ajiweke katika mazingira mazuri ya kupata nafasi ya kwenda kucheza soka nje ya nchi

Balama aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea klabu ya Allince Fc, amekuwa katika kiwango cha juu jambo lililomuibua kocha wa zamani wa Stand United Athumani Bilali 'Bilo' ambaye kwa sasa anainoa Gwambina Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza

Bilo amemtaja Balama kama mchezaji wake bora kwenye ligi kuu msimu huu, akimtaka aongeze juhudi zaidi kwani anaweza kupata nafasi kwenda kucheza soka nje ya nchi hasa barani Ulaya

"Balama ni miongoni mwa wachezaji wa ligi kuu wanaojituma sana ndani ya uwanja. Nimekuwa nikimfuatilia katika mechi mbalimbali ambazo amepangwa, ni mchezaji anayetimiza majukumu yake kikamilifu"

"Ukiniuliza mchezaji bora kwangu kwenye ligi ni yupi, lazima nikwambie ni Balama kwani ni mmoja wa wachezaji bora niliowahi kuwashuhudia. Anajituma, pia ni mchezaji asiyechoka uwanjani," Bilo alinukuliwa na Mwanaspoti

Bilo ambaye ameiweka Gwambina Fc katika nafasi nzuri ya kupanda ligi kuu, amesema Balama amebakisha muda mfupi kabla ya kupata nafasi nje ya nchi kama ataendelea kufanya vizuri

Bilo ni kocha wa pili kumtabiria Balama mambo makubwa kutokana na mambo anayofanya uwanjani

Aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye ndiye aliyemsajili, alimtaja kiungo huyo kama miongoni mwa wachezaji wachache Watanzania ambao wanaweza kwenda kucheza soka barani Ulaya

Wakati akiwa Yanga, Zahera alimtumia Balama katika nafasi mbalimbali ikiwemo beki wa kulia kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United ambao ulipigwa uwanja wa Taifa

Zahera alimsifu Balama kuwa ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani jambo ambalo linampa kocha wigo mpana hasa pale timu inapokuwa na mapungufu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’