Chama cha soka cha Guinea kimefuta msimu wa 2019-20 kutokana na janga la corona
Aidha vilabu vyote vilivyokuwa vikishiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza nchini humo, vimekubaliana msimu umalizwe bila ya kuwa na bingwa wala timu kushuka au kupanda daraja
Klabu ya Horoya Ac ambayo anacheza mshambuliaji wa zamani wa Yanga Heritier Makambo, ndio iliyokuwa ikiongoza ligi wakati hatua za kuisimamisha zilipochukuliwa na Serikali ya Guinea kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa corona
Makambo anahusishwa kuwa mbioni kurejea Yanga, pengine uamuzi huu utaharakisha mpango wa GSM kumvuta nyota huyo Jangwani
ADVERTISE HERE