Sitabomoa kikosi - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 May 2020
Sitabomoa kikosi - Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema mapendekezo yake ya usajili yamezingatia maeneo ambayo yana mapungufu tu, na sio kusajili wachezaji wengi

Eymael ambaye bado amekwama huko Ubelgiji kutokana na changamoto ya janga la corona, amesema ameridhishwa na viwango vya wachezaji wengi aliowakuta hivyo marekebisho atakayofanya sio makubwa

"Nimewasilisha ripoti ambayo ina mahitaji kwa nafasi husika, huwezi kubomoa kikosi kwa kiwango kikubwa, timu ni nzuri na inahitaji maboresho kidogo tu hivyo nikipata wachezaji saba bila shaka nitakuwa na kikosi imara sana msimu ujao," Eymael aliuambia mtandao rasmi wa klabu ya Yanga

Hata hivyo Eymael amesema michakato yote ya usajili itawekwa hadharani pale dirisha la usajili litakapofunguliwa, kwa sasa hawezi kuweka hadharani majina ya wachezaji aliopendekeza wasajiliwe

"Kwa sasa hatuzungumzii usajili, tunazungumzia mapendekezo tu, kwa hiyo nimewasilisha kwa uongozi na ninaamini wao watafuatilia kwa kila mchezaji kwa mujibu wa taratibu za usajili ili kuona nani tunaweza kumpata na nani hatuwezi na mbadala wake atakuwa nani"

Eymael amedhamiria kukisuka upya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kipiga hesabu ya kutwaa ubingwa msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’