Fei Toto ataja kilichokwamisha mpango wa kutimkia Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2020
Fei Toto ataja kilichokwamisha mpango wa kutimkia Misri

Kiungo fundi wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' amesema klabu ya Smouha Fc inayoshiriki ligi kuu ya Misri iliyokuwa ikimtaka akafanye majaribio, haikuwa imewasiliana na yeye moja kwa moja

Smouha iliwataka Fei Toto na Ditram Nchimbi waende kufanya majaribio kabla ya kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael kugomea wachezaji hao kuondoka wakati timu ikikabiliwa na mechi muhimu

"Smouha hawakuwasiliana na mimi moja kwa moja, waliwasilian na viongozi wa Yanga, maamuzi yalifanyika kwenye ngazi ya uongozi, " amesema

Hata hivyo Fei Toto amefichua kuwa bado ana ndoto ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, anaamini ataondoka wakati wake ukifika

"Natamani sana kwenda kucheza soka nje ya nchi, hiyo ni ndoto yangu ya muda mrefu naamini siku moja nitafanikiwa"

"Sasa nina nafasi nzuri zaidi ya kukamilisha ndoto hiyo hapa Yanga kwani naonekana zaidi kuliko nilipokuwa nikicheza Zanzibar," amesema

Fei Toto alianza msimu kwa kusuasua lakini alirejea kwenye kikosi cha kwanza kwa kishindo kwenye mechi nne mfululizo kabla ya Serikali kuchukua hatua ya kusimamisha ligi kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona

Kwa sasa yuko visiwani Zanzibar akiaendelea kufanya mazoezi binafsi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’