Mahadhi aahidi makubwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2020
Mahadhi aahidi makubwa Yanga

Winga wa Yanga Juma Mahadhi amesema bado ana nafasi ya kudhihirisha ubora wake mbele ya mashabiki wa timu hiyo baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa karibu miaka miwili

Mahadhi aliyekuwa akitabiriwa kuwa Msuva wa baadae Yanga, amesema bado ana kazi ya kufanya ndani ya kikosi cha Yanga

Aidha nyota huyo amefichua kuwa uongozi wa timu hiyo umeonyesha imani kwake baada ya kumuongezea mkataba hadi mwaka 2022

"Nashkuru kwa sasa hali yangu ni nzuri, nafahamu nina deni kubwa kwa mashabiki wa Yanga kwani hawajaniona uwanjani kwa muda mrefu"

"Ninao muda wa kutosha kuwapa burudani, kikubwa ni kuombeana uzima na afya" amesema

Mara ya mwisho Mahadhi kuonekana dimbani ilikuwa August 19 kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 2-1

Mahadhi alipata majeraha makubwa ya goti katika mchezo huo ambapo alilazimika kufanyiwa upasuaji wa goti mara mbili

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’