Baada ya Rais Dk John Magufuli kudokeza kusudio lake la kurejesha ligi kuu, mashabiki wanasubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe ya michuano hiyo kurejea
Jana TFF wametoa taarifa kuwa wanaendelea na michakato ya ndani ili kuweka taratibu sawa na wakati huohuo wakisubiri ruhusa rasmi ya Serikali waweke gozi uwanjani
Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 51, ina mechi 11 za viporo kuweza kumaliza msimu huu
Mabingwa hao wa kihistoria pia wanakabiliwa na mchezo wa robo fainali kombe la FA, droo ya hatua hiyo ikiwa bado haijapangwa
Katika mechi 11 za ligi zilizobaki, mechi tano zitapigwa jijini Dar es salaam na nyingine sita kupigwa mikoani

ADVERTISE HERE