Maradhi yaliniondoa kikosi cha kwanza - Bui

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2020
Maradhi yaliniondoa kikosi cha kwanza - Bui

Kiungo mkabaji wa Yanga Abdulaziz Makame 'Bui' amesema changamoto ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza inamfanya azidi kupambana ili kumshawishi mkufunzi wa Yanga Luc Eymael

Makame alianza vyema maisha yake Yanga akijihakikishia namba wakati mabingwa hao wa kihistoria wakinolewa na Mwinyi Zahera na baadae Charles Mkwasa kama kocha wa muda

Hata hivyo tangu alipotua Eymael mwezi Januari mwaka huu, nafasi yake imekuwa finyu

Kiungo huyo mwenye sifa ya kupiga pasi ndefu zenye uhakika, amesema alikaa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na maradhi jambo lililomnyima nafasi ya kuonekana mwanzo na kocha Eymael wakati alipoanza majukumu yake

Makame amesema sasa yuko sawa, tayari kupambana kuhakikisha anamshawishi Eymael kuweza kumjumuisha kwenye kikosi chake

"Suala la mimi kutopata nafasi nalichukulia kama changamoto ya kunifanya nipambane zaidi. Matatizo ya kiafya ya kuumwa ni moja ya sababu iliyochangia kushindwa kumshawishi kocha kunipanga kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa kwa kocha aliyepita Mwinyi Zahera, "

"Bado naamini uwezo wa kila kocha kwa kuwa kila mmoja anakuja na mfumo na mbinu zake, mimi kama mchezaji natakiwa kupambana kutimiza majukumu yangu mazoezini na nina uhakika kurejea kwenye kikosi cha kwanza chini ya Eymael," alisema Makame

Kiwango alichokuwa nacho mwanzoni mwa msimu kilimfanya kocha Etienne Ndayiragije amjumuishwe kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichofanikiwa kukata tiketi ya kushiriki fainali za CHAN zitakazofanyika Cameroon mwakani

Baada ya kuondoshwa kwa taabu na Zesco United kwenye michuano ya ligi ya mabingwa raundi ya kwanza, Mkufunzi wa Zesco George Lwandamina alimtaja Bui kuwa ni miongoni mwa wachezaji waliomvutia kwenye kikosi cha Yanga

Lwandamina aliyewahi kuinoa Yanga, alimtaja Bui kuwa mchezaji mwenye nafasi ya kufanikiwa kama ataendelea kujituma kutokana na umri wake bado kuwa mdogo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’