Beki wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa Stephano Mwasika amesema uongozi wa timu hiyo unaweza kutumia mbinu za makocha na viongozi waliiopita katika kuimarisha nafasi zenye mapungufu
Mwasika amesema enzi zao wakati wanacheza Yanga, ilikuwa mchezaji anayesajiliwa kwa nafasi fulani, lazima mchezaji aliyepo ambaye anayecheza nafasi ile kwa ufasaha atoe ushauri au kupendekeza mchezaji anayefaa.
Katika kipindi chake, Mwasika amesema alipendekeza kusajiliwa kwa David Luhende, beki ambaye baadae alikuja kufanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga
Luhande kwa sasa anaitumikia klabu ya Kagera Sugar akiwa miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri kwenye ligi
Mwasika amesema hata ujio wa Juma Abdul lilikuwa pendekezo la aliyekuwa nahodha wao wakati huo ambaye alikuwa akicheza namba mbili, Shadrack Nsajigwa
Abdul alisajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Mtibwa Sugar
Inaelezwa uongozi wa Yanga bado unaendelea kutumia utaratibu huo wakiwashirikisha wachezaji waandamizi kwenye baadhi ya usajili
Mfano ni suala la nyota wa Coastal Union anayetajwa kuwaniwa na Yanga Bakari Mwamnyeto ambaye mkongwe Kelvin Yondani aliwashauri mabosi wake wamsajili kwani anaweza kuwa mbadala wake hapo baadae