Msuva haoni timu ya kuipoka Yanga ubingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2017
Msuva haoni timu ya kuipoka Yanga ubingwa
Licha ya kuwa nchini Morocco, winga Simon Msuva amesema huwa anaifuatilia kwa ukaribu ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na ameitabiria Yanga, timu aliyoichezea kwa misimu mitano itahifadhi ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo.

Tofauti na misimu mingine, Msuva amesema msimu huu ligi inaonekana kuwa na ushindani zaidi kwani kila timu inaonekana kujipanga vizuri.

Yanga ilianza ligi kwa kusuasua lakini sasa iko nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC na Simba ikiwa na alama 17, alama mbili nyuma ya vinara hao wenye alama 19 kila mmoja.

"Naifuatilia ligi kupitia simu yangu ya mkononi," amesema Msuva ambaye yuko kwenye kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin.

"Pamoja na ushindani kuonekana kuwa mkubwa, bado Yanga ina nafasi ya kutetea taji lake kwa msimu wa nne."

"Licha ya mimi pamoja na wengine walio-ondoka, Yanga imefanya usajili makini kwani sasa wachezaji wameanza kuelewana na timu inarejea kwenye hali yake ya ushindani."

"Miaka yote ni kawaida ya Yanga kuanza ligi kwa kusuasua lakini kadiri siku zinavyosogea ndio timu inavyozidi kuimarika."

"Msimu huu nao hauna tofauti sana," amefunguka Msuva.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’