Yanga mpya kila mmoja lazima awajibike

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 May 2020
Yanga mpya kila mmoja lazima awajibike

Wadhamini wahisani wa klabu ya Yanga kampuni ya GSM wamesema mabadiliko ya usimamizi wa timu hiyo ndio jukumu la kwanza ambalo linapaswa kufanywa kuelekea mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga

KYanga imetangaza kuanza kwa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wake wa uendeshaji zoezi ambalo litafanyika kwa awamu nne

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema ili timu iweze kuendeshwa kisasa lazima kila idara iwajibike

"Maboresho ya usimamizi wa klabu tunamaanisha kila idara inapaswa kuwajibika kuingiza pesa ambazo zitachangia kwenye uendeshaji wa timu," amesema Said

Said ameongeza kuwa hata kitengo kinachohusika na wachezaji lazima wahakikishe timu inakuwa na wachezaji bora ambao wanaweza kuuzwa kwa timu nyingine na kuiingizia klabu mapato

"Baada ya mauzo ya mshambuliaji Heritier Makambo kwenda Horoya AC, sidhani kama Yanga iliuza mchezaji mwengine na kupata faida. Jambo hilo tunataka kulibadilisha"

"Pia tutatengeneza kanzidata ambayo itawasaidia wale wanaotaka kuja kuwekeza kwenye klabu ya Yanga. Tunahitaji kufahamu idadi ya Wanachama tulionao na mchango wao kwa timu"

"Kila Mwekezaji anayetaka kuja atahitaji kufahamu kwa kiasi gani wanachama wa klabu wanachangia maendeleo ya timu yao, pia atahitaji kuwekeza sehemu ambayo atakuwa na uhakika wa kutengeneza faida"

GSM wamejitosa kuhakikisha wanaifanya Yanga iendeshwe kisasa kwa kuajiri wataalam kutoka barani Ulaya kusaidia kuweka sawa mfumo mpya wa uendeshaji

"Tunataka kuona timu yetu inaendeshwa kisasa ndio maana tumechukua wataalamu kutoka Ligi Kuu ya Hispania, La Liga kutusaidia kufikia malengo yetu. Tumejifunza kutokana na makosa waliyofanya wenzetu ndio maana tunataka kufanya kitu tofauti"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’