Kulingana na mtandao wa soka nchini Ghana unaofahamika kwa jina la Football Ghana, mabingwa wa kihistoria Tanzania, klabu ya Yanga imejitosa kumuwania mshambuliaji wa Asante Kotoko Yacouba Sogne ambaye amemaliza mkataba kunako klabu hiyo
Awali Sogne alikuwa akitajwa kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Medeama ya hukohuko Ghana hata hivyo dili la uhamisho wake lilisitishwa baada ya Medeama kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa
Kwa hapa Tanzania, Simba wanadaiwa kuwa klabu ya kwanza kuwasilisha ofa kumtaka mchezaji huyo lakini Yanga wamejitosa wakiwa na ofa nono zaidi
Kulingana na mtandao huo, ofa ya Simba waliyotoa ni $80,000 huku Yanga wakipanda juu kwa dau la $100,000
Aidha kuna taarifa kuwa nyota huyo pia anawaniwa na klabu ya Orlando Pirates
Katika jitihada za kuboresha kikosi chake, Yanga imeweka mkazo katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambapo nyota kadhaa wamekuwa wakihusishwa na mabingwa hao wa kihistoria
Washambuliaji wengine wa kigeni wanaohusishwa na Yanga ni Heritier Makambo (Horoya AC) na Michael Sarpong (huru)